Udadisi wa Wanafunzi wa Ilboru kuhusu Jua na Nishati yake

Maswali ya udadisi hapo chini kuhusu Jua na Nishati yake yameulizwa na wanafunzi wa shule ya Msingi ilboru mkoani Arusha katika Club ya sayansi baada ya kujifunza kuhusu Nyota ya Jua. Kupitia kipindi hiko wanafunzi pia walichunguza na kulitazama jua kwa kutumia miwani maalumu ya kutazama Jua (Solar Eclipse Shade) pamoja na vifaa vingine kama Solar Prism. 

Unaweza kushirikiana kwa kujifunza pamoja na wanafunzi hawa kwa kujibu maswali hapo chini au kwa kushirikiana nao kwenye mjadala kuhusu maswali haya na mengine. Ili kufanya hivyo unaweza kuwasiliana na mwalimu wao Bwana Eliatosha Maleko kwa kupitia eliatosha@gmail.com

  1. Clara Elirehema aliuliza:

           Hapa duniani yako madini mbalimbali ambayo ni muhimu sana katika kuzalisha vitu mbalimbali, je wataalamu hawaoni umuhimu wa kutumia gesi zitokanazo na jua kama gesi ya Hydrogen ambayo ni zaidi ya asilimia 92, Hellium asilimia 83 zinazounda jua?

  1. Rebeca Abraham aliuliza:

       Je ni vifaa gani hutumika kulichunguza na kulipima jua na je, ni vifaa kutoka mataifa gani?

  1. Caren James aliuliza:

     Tunajifunza kuwa wapo wanasayansi na nchi mbalimbali duniani zilizotumia na kupeleka Satelite angani pamoja na wanasayansi katika Mwezi, Je katika nyota jua wapo wanasayansi waliowahi kwenda na je kwenye nyota jua kuna ardhi kama ilivyo duniani?.

  1. Maliki Abasi aliuliza:

    Upepo wa jua una faida gani kwa viumbe hai au madhara gani ikiwa utafika duniani?.

  1. Neema Florence aliuza:

Tumejifunza kuwa umri wa nyota jua ni miaka Bilioni 4 na nusu, Je umri wa jua unapimwaje ? Na je, jua linazeeka au kupunguza mwanga wake au nguvu yake kuanzia lilipoumbwa?

  1. Noela Erick aliuliza:

     Katika masomo ya Jiografia na Sayansi tumejifunza kuwa Nishati huweza kuhifadhiwa kwa muda mrefu, Je mataifa duniani mwote  hayaoni umuhimu wa kuwa na hifadhi kubwa ya nishati itokanayo na jua kama wanavyohifadhi nishati ya mafuta kama vile Petroli, dizeli na mafuta ya taa?

  1. Aneth Aristides aliuliza:

    Nini maana ya Nuclear  fussion, na je ina umuhimu gani  katika maisha yetu ya kila siku?

  1. Emaculata Pauli aliuliza:

     Tumejifunza kwamba jua linatoa joto zaidi ya nyuzi Bilioni za joto na sehemu ya uso wake hutoa joto nyuzi 6000°C, je ni kwanini katika Viwanda vikubwa duniani havitumia joto la jua katika kuyeyusha vyuma vizito na vitu vingine   vinavyohitaji joto kubwa ili kuyeyushwa?

 Wapendwa haya ni baadhi tu ya maswali  yatokanayo na kipindi hicho  ni matumaini yetu kuwa majibu yenu yatatupatia uelewa zaidi. 

Leave a Reply