Maswali ya Wanafunzi Kuhusu Satelaiti

Kipindi cha macho angani kuhusu satelaiti kimeiubua maswali mengi toka kwa wanafunzi mengi kuhusu satelaiti na umuhimu wake kwa maisha ya leo. 

Maswali hayo yamepatiwa majibu, nasi tumeona ni vyema kushiriki nanyi ili tujifunze pamoja.

Wanafunzi wa shule ya Msingi Ilboru wakiongozwa na mwalimu wao Eliatosha  Maleko, wamekuwa wakijifunza kuhusu elimu ya anga au astronomia kupitia vipindi vya redio vijulikanavyo kama macho angani.

Vipindi hivi vinapatikana kupitia mtandao kwa kubofya hapa na kisha kuchagua mada ambayo ungependa kujifunza zaidi.

Kipindi cha tarehe 20 Mwezi wa saba, wanafunzi walipendelea kujifunza kuhusu satelaiti na umuhimu wake. Maswali mengi yaliulizwa na wanafunzi kuhusu satelaiti kama yalivyo nakiliwa hapa chini.

Tupe maoni yako juu ya mada hii na pia kama wanafunzi katika shule yako wanaweza kuwa na maswali tofauti au zaidi kuhusu satelite.

Unaweza pia kushiriki nasi majibu ya maswali haya kwa kuandika kwenye sehemu ya maoni au comment. 

Walter Bernard
-Satelite imeundwaje?
-Kwanini satelite inapoanguka hupata msuguano mkubwa?

Emma Loy
-Kwanini satelite ni kubwa kama Lory?
– Kwanini mwezi ni satelite ya asili?
– Kwanini satelite hufungwa katika roketi?

Nestor Alex
-Obit Nini?
-Kwanini satelite ina mwendo wa haraka ikiwa Angani?

Ester Jonathan
-Gps ni nini?
-Satelite ni nini?

Diana Charles
-Satelite ikianguka katika makazi ya watu nini kitatokea?

Ester Mahubiri
-Kwanini usafiri wa ndege unategemea sana mawasiliano ya satelite?

Abigael Abrahamu
-Katika Satelite je! Kuna Binadamu wanaoishi humo?

Nengarivo
-Kwanini satelite huwaka kwa kutoa mwanga inaokimbia?

Merry Alex
-Wakati wa kuanguka kwa satelite hutokea nini?

Paschal David
-Satelite inatengenezwa je?
-Zipo aina ngapi za satelite? satelite ya kwanza kurushwa angani ni ipi na ilikuwa ina madhumuni gani?

Editha Francis
-Kwanini Satelite huwekwa Angani?
– Kwanini Satelite huwekwa Angani na sio ardhini?
-Satelite zina umuhimu gani kwa maisha yetu ya kila siku?

Deborah Adam
-Kwanini usiku kuna kua na nyota nyingi angani kuliko mchana?
-Kwanini bila Gps mambo mengi katika dunia yetu ya kisasa hayaendi?
– Kwanini satelite ikiwa angani ni ndogo kama nyota?
-Kwanini vifaa vya usafiri wa anga kama vile ndege huratibiwa na satelite?
-Satelite zina umuhimu gani kwa maisha yetu na viumbe wengine duniani?
-Je kwanini satelite nyingi huzunguka Sayari yetu ya tatu ya dunia?

Eliatosha
-Elimu ya Astronomia ina faida gani kwetu?
-Kwanini satelite huzunguka dunia kupitia obit na sio njia nyingine?
-Nguvu za jua zina geuzwa VIP kubwa Umeme?

Belinda Abihudi
-Kwanini satelite nyingi hutumia obit?
-Kwani satelite huzunguka dunia kwa kilometa ngapi?
-Kwanini vyombo vya habari haviwezi kufanya kazi bila satelite?

Norine Nelson
-Kwanini satelite nyingi haziwezi kukaa sehemu moja?
-Kwanini satelite kukimbia kwa kasi kubwa sana?

Leillah Abdillah
-Kwanini binadamu wanategemea days za Satelite?
– Kwanini satelite zinazorushwa karibu angani huanguka mapema zaidi?
-Ikiwa Satelite zitashindwa kufanya kazi je nini kitatokea duniani?

Anna Joseph
-Satelite huanguka kwa sababu gani na wapi?
-Kuna aina ngapi za Satelite?
-Rocket zinazorushwa angani hukaa huko kwa a muda gani?
-Satelite huongozwa na nani?
-Kwanini satelite ziko maelfu angani na sio moja?

Andreas Dismas
-Kwanini satelite kwenye Obit ya karibu haziwezi kuendelea na huanguka
dunia?
-Kama satelite za kutengenezwa na binadamu iliharibika je! satelite ya asili
si itaendelea kutuma taarifa/days na kuzalisha umeme?

Nickson Jonas
-Je satelite hutumia vifaa gani na vingapi?

Brayan Leonard
-Amesema kuna hewa inayorekebisha mwelekeo wa satelite ni hewa gani hiyo?
-kwanini satelite zinatofautiana majina na je? Kazi zake ni moja?
-Rocket ina kazi gani angani?
-Satelite ziko ngapi na je?kazi zake hutofautiana?
-je satelite zinapoanguka hazidhuru watu au huwekwa sehemu maalumu la
kuanguka?
-Je? Satelite haidhuriki na mwanga wa jua angani?

William Roman
-kwanini rocket huruka mpaka anga la nje?
-Kwanini satelite hukaa angani bila kuanguka?
-kwanini satelite hazikai katika makazi ya binadamu?
-kwanini satelite haziwezi kuonekana mchana kama zinavyooneka usiku?

Leave a Reply